Hatimaye uorodheshaji wa timu katika makundi mbalimbali ya Kombe la Dunia utakaoanza mwaka ujao Juni ilikamilika ijumaa iliyopita.Timu zote thelathini na mbili ziligawanywa katika makundi manane ambapo kila kundi ilipewa timu nne.Kama kawaida kuna wale wanafurahia mchakato huo ila hakutawahi kosekana wanaohuzunika pia kwani matarajio yetu huwa tofauti huku kila mmoja akilenga timu wanazozidi ili kuwashinda na kuendelea katika awamu zifuatazo.
Katika shughuli hiyo,timu za Afrika zimepewa mapinzani dhabiti,swala ambalo linatupa wasiwasi ni iwapo kuna timu yoyote kutoka bara hili itafaulu kuvuka awamu ya makundi.Acha tutizame nafasi ambazo timu zetu zinazo katika makundi yao.
1.KAMERUNI
Iwapo kuna timu ya Afrika ambayo imenyimwa nafasi kabisa basi ni taifa la Kameruni.Kama shabiki sugu wa timu hii,itanibidi nivumilie niombe angalau tusiondolewe bila pointi katika kundi hili la A.Kucheza dhidi ya waandalizi Brazil,Korasia na Meksiko si suala la kutilia hamnazo.
Mibabe hawa wa soka barani watalazimika kutia bidii na kuomba miujiza itendeke katika michezo yao maanake hakuna asiyefahamu ukali wa Brazil hasa kama waandalizi wa kombe hili na iliyosheheni magwiji kama Neymar,Luiz,Ramirez,Dani Alves,Paulinho,Silva n.k.Meksiko pia inawachezaji wa ngazi ya juu wakiwemo Chicharito na Dos Santos,bila kusahau Korasia inayojivunia Modric,Olic na Mandzukic.Eto'o,Song,makoun na Mbia watahitaji kujituma zaidi maanake nafasi ya tatu ndiyo bora zaidi wanayoweza kupata katika kundi hili.
2. COTE D' IVOIRE
Kando na wenzao Kameruni,timu ya Ivory Coast pia ina mlima wa kukwea katika kundi la C itakapochuana na kolombia,Ugiriki na Japani.Timu hizi ni za haiba kubwa ulimwenguni na zinajivunia magwiji katika mchezo huu.
Kolombia itawategemea Falcao na Rodrigez kujinasua ilahali Ugiriki itamwangazia mlinzi Samaras na Gekas kufuzu awamu ijayo.Timu ya Japani pia ina wachezaji kama Kagawa,Honda na Okazaki ambao watajituma kufuza kutoka kundi hili.Ni wakati Drogba,Yaya Toure na Kolo Toure kujikakamua zaidi ili wainasue bara hili.Nafasi bora ninayowapa majabali hawa wa Afrika ni ya tatu.
3. NAIJERIA
Tofauti na wenzao,timu ya Naijeria haijabanwa sana katika makundi kwani mapinzani wao si wenye haiba kubwa kando na Ajentina. Kundi hili la F linasheheni Naijeria,Ajentina,Uajemi na Bosnia.Ama kwa kweli,uongozi wa kundi hili lina mwenyewe,Messi na wenzake,lakini nafasi ya pili bado ni wazi kwa timu tatu zilizosalia.Naijeria ndiyo timu pekee ya Afrika ambayo inaweza kutuwakilisha angalau katika awamu ya kumi na sita bora ila sitarajii wao kuzidi hatua hiyo.Mikel,Matin na wenzao watumie nafuu waliopewa katika kundi hili angalau kufuzu hatua nyingine.Uajemi na Bosnia hawajaonyesha ukali wowote katika soka ulimwenguni na iwapo kutakuwa vihi hivi,basi Naijeria itaungana na Messi na wenzake kutoka kundi hili.
4. GANA
Timu ya msimu huu wamejipata katika mikono hatari baada ya kuorodheshwa na Ujerumani,Ureno na Marekani katika kundi la G.Kuna wengi tayari wamefutilia mbali uwezekano wa timu hii kufuzu kutoka kundi hili ila kunao wachache wenye matumaini ya kufana kwa Gana.Jambo lililowazi ni kuwa mapinzani wake si wa kumalizia vinyang'anyiro hivi kwenye makundi ila katika hatua za mbele.
Nuer,Muller,Schwistiger,Lahm na Gomez wataiongoza Ujerumani kama kawaida huku Ronaldo na Nani wakiwakilisha Ureno.Dempsy na Bradely wataiongoza nchi ya Marekani huku Gyan na Essien wakijitahidi kuiokoa timu yao kutoka kwa janga hili.Vile vile,timu ya Gana ninaipa nafasi ya tatu kama yao bora zaidi.
5. ALJERIA
Kama ilvyo na wenzao,timu hii kutoka kusini mwa Afrika watapata wakati mgumu kujinasua kutoka kundi hili la mwisho H pale watakapochuana na Ubelgiji,Urusi na Korea Kusini.Timu ya Ubelgiji imepata umaarufu siku chache zilizopita kwa kuwa na wachezaji hodari kama Fellaini,Vamalean,kompany,Hazard,De Bruyne na courtois.Urusi inajivunia Shirokov na mlinzi Akinfeev pamoja na kocha wao Capello.Korea Kusini inao Jacheol na Lee Keunho.Watakaotegemewa na Aljeria ni pamoja na mlinzi shupavu Mandjid,Sofiane na Medhi.
Mtazamo wangu ni ule ule,nafasu bora ya timu hii kunyakua kutoka kundi hili litakuwa ya tatu ila itabidi wajitume zaidi ili kufikia hapo.
Uchambuzi huu unaashiria kuwa kati ya timu tano za Afrika,timu yenye nafasi bora ya kufuzu na kutuwakilisha katika awamu ya kumi na sita bora ni Naijeria.Wimbo utakuwa ni ule ule,tushabike timu zetu ila kombe tuwaachie wenyeji.Kila la heri timu za Afrika katika maandalizi yenyu.
No comments:
Post a Comment