Monday, 2 December 2013

KELI ANATOSHA


Keli akimbia na mpira katika mojawap
 ya michuano ligini

Wapenzi wote wa soka nchini hasa wanaoshabikia timu ya taifa Harambee Stars watakubaliana nami kuwa timu yetu imekuwa ikimkosa mshambulizi wa kuziba pengo lililoachwa na Denis Oliech ambaye mchezo wake umedorora kwa michuano kadhaa iliyopita.Aidha,si kwamba hakukuwa na mshambulizi yeyote katika miaka iliyopita ila tu kati ya waliokuwemo,hamna aliyeonyesha ukakamavu katika safu hiyo.Oliech ni mshambulizi bora nchini na si kwa sababu yake kucheza ulaya ila mabao na michango ambayo ameipa timu ya taifa ndiyo inampa uzito huo na hii ndiyo maana anazidi kuitwa kwenye kikosi cha Harambee Stars hata ingawa umri wake umekolea.
                        

                                                     
JAWABU
Hata hivyo utaafikiana nami kuwa uhaba huu tayari unafika ukingoni kila tukimsikia Jacob Keli.Juzi nikitizama mchuano kati ya timu yetu na Sudan Kusini,shabiki mmoja alizungumza kwa sauti na kusema kuwa Oliech hatapata nafasi kwenye kikosi cha timu hiyo tena.Shabiki huyu hakuwa mbaguzi ila mchezo wake Keli ndio ulimchochea kusema hayo.Ni washambulizi wangapi wameonekana kutwaa nafasi hiyo ila kutupotezea matumaini?Si John Baraza,Mike baraza,Francis Ouma,Kemboi,Obadiah Ndege,Geoge'Black Berry',Lavatsa,Wanga,Were n.k.Orodha hii ni ndefu ila hakuna kaiti yao aliyetupa kiburi cha safu ya ushambulizi kama Oliech.Japo Were bado hajachezeshwa katika timu ya taifa,lakini hivi sasa,mkombozi wetu ni Jacob Keli.

                                                             Kazi zake

Keli apokea tuzo la mfungaji bora ligini
Hatumzungumzii Keli kwa sababu waliojaribu hapo awali walishindwa ila ni kwa ajili ya kazi aliyoifanya.Msimu uliopita,Keli alikuwa mfungaji bora wa ligi ya taifa kwa mabao kumi na saba,mabao mawili mbele ya mwenzake wa Tusker Jese Were.Isitoshe, Keli alitawazwa mshambulizi bora ligini na hatasahaulika kwa kuwanyanyasa mabeki wa Gor Mahia kwenye mchuano wao wa mwisho ligini ambapo alifunga bao moja na kukosa nafasi nyingi ingawa walishinda kwa mabao mawili bila jawabu.Hivi maajuzi,Keli pia alijitoa mhanga kusaidi nchi hii kuilaza Sudan Kusini.Katika mchuano huo,Keli alifunga bao moja na kuwasumbua mabeki wa mapinzani kila mara akiwa na mpira.

Dimba la CECAFA bado linaendlea na iwapo tutautwaa ubingwa huo,basi itakuwa ni usaidizi wa Keli.Mkufunzi wa taifa adel Amrouche anafaa kumtumia mshambulizi huyu hasa kwa kumwanzisha maanake mechi yetu na Ethiopia ambayo tulitoka sare ya kutofungana,Keli alichezeshwa kipindi cha pili ingawa haikumtosha kujituliza na kuonyesha makali yake.Ninatumai kocha huyo atamtumia vilivyo maanake kufikia sasa,KELI ANATOSHA.


                        

No comments:

Post a Comment