Mara ya mwisho timu ya taifa kutwaa kombe lilikuwa mwaka wa 2002 ambapo tulinyakua kombe la CECAFA chini ya uongozi wa Musa Otieno kwenye ulinzi.Lakini baada ya kutwaa kombe hili tena chini ya uongozi wa David Owino 'Calabar' katika safu ya ulinzi,sina shaka kuwa yeye ndiye mridhi halali wa viatu vya sogora Musa.Katibu Mkuu wa klabu ya Owino,Gor Mahia,George Bwana aliwahi kunukuliwa akisema kuwa mchezaji huyu atasalia katika historia ya nchi hii kwani mchezo wake ni wa hali ya juu.
Owino alianza mchezo huu katika akademia ya nakuru All Stars mwaka wa 2004-2008,iliyokuwa ikifahamika kama St. Joseph.Alijiunga na klabu ya Karuturi mwaka wa 2008 hadi 2011 aliposajiliwa na miamba wa soka nchini Gor Mahia.Mchezo wake ulivutia timu ya taifa na kuitwa kwenye vikosi mbalimbali.Mojawapo ya michuano ambayo alifana zaidi ni kati ya Nijeria ambapo alimkaba mshambulizi Mosses na kumnyima nafasi ya kutuadhibu nyumbani kwao.Baada ya mchuano huo,mlinzi wa taifa Arnold Origi alimmiminia sifa tele mchezaji huyu kwenye kurasa ya kitandazi 'Kenya imebarikiwa kuwa na walinzi bora enzi hii,David Owino na David 'cheche' Ochieng'
Ubabe wa mchezaji huyu haikukomea hapo kwani aliisaidia Gor kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tusker kama mlinzi wa kulia.Pia alisimama kidete na kuwadhibiti washambulizi pinzani kwenye dimba la CECAFA akiwemo mfungaji bora kwenye kitupe hicho wa Sudan,Salah ambayo Kenya ilishinda.Hivi majuzi ametajwa kama mchezaji bora wa goal.com na hivyo kuashiria uwezo wake wa kuisaidia timu hii katika awamu zingine.Mlinzi huyu amepata sifa si haba kutoka kwa wakufunzi mbalimbali,wachezaji na hata baadhi ya wadadisi wa soka nchini.Ama kwa kweli,tukiwa na Owino,ni nini kitatuzuia kushiriki dimba la kombe la bara Afrika na hata kufanya vyema katika shindano hilo?
No comments:
Post a Comment